JE, ULIWAHI KUFIKIRIA UWEZO WA KUSIKIA WA SIKIO LAKO?

Unapojitazama katika kioo unaona masikio yako maridadi sana. Wengine huyaongezea urembo kwa kuyawekea hereni zenye maumbo mbalimbali. Bila shaka unajivunia kuwa na masikio mazuri.baby face on mirror

Sasa nawakaribisha katika makala hii nzuri, natumaini itakuvutia na utajifunza jambo zuri kuhusu masikio yetu.

Ukweli uwezo wetu wa kusikia ni wa kipekee sana.Bila shaka unafurahia kusikiliza mdundo mzuri wa muziki, sauti tamu za ndege porini au wanapokuwa karibu na nyumba zetu na hata sauti nzuri za ndugu zetu wapendwa nyumbani au kupitia simu.
sound wave
Uwezo wetu wa kusikia unatufanya tuweze kukadiria umbali wa sauti, uzito wa sauti na upande inapotokea sauti hiyo. Wataalamu wa mfumo wa neva wanasema sikio lenye afya linaweza kusikia mawimbi ya sauti ya Hezi 20 hadi 20,000.

Hezi ni idadi ya mizunguko ya mawimbi ya sauti kwa sekunde moja. Sikio letu linaweza kusikia vizuri zaidi mawimbi ya sauti ya Hezi 1,000 hadi 5,000.

Tuweza pia kutambua ikiwa hezi moja imepungua, yaani badiliko la mawimbi ya sauti. Kwa mfano: ulikuwa ukipokea mawimbi ya sauti yenye hezi 500 kisha kukatokea badiliko la hezi moja ya mawimbi ya sauti, basi utapokea hezi 449. Na kadiri hezi zinapopungua ina maana kuwa sauti inayopokelewa na sikio huwenda ikawa umbali Fulani toka ulipo.

Kwa hiyo tunza sana masiko yako dhidi ya sauti kali zinazoweza kuharibu uwezo wetu mzuri wa kusikia. Uwe na kawaida ya kuyasafisha kwa kutumia kijiti chenye pamba laini au kitambaa chenye ncha laini ili kuondoa uchafu katika masikio.

Natumaini umefurahia makala hii fupi kuhusu masikio yetu.
Kwa leo, naishia hapa. Je, una maoni kuhusu habari hii? Karibu uchangie na kuboresha pia.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s