MWILI WAKO NI MASHINE YA KIPEKEE SANA. WAJUA KWANINI?

Je, uliwahi kujiuliza kwanini unaweza kusimama au kutembea pasipo kuanguka? Na ni nini basi kinakusaidia usimame au utembee kwa urahisi bila kuanguka?

Nakukaribisha ufuatane nami katika makala hii, na hapa utapata majibu ya maswali hayo juu.  Bila shaka utafurahia kujua jinsi jambo hilo linavyotukia.

Ukweli ni kwamba mwili wetu ni kama mashine tata yaani ni mashine ya kipekee sana na utendaji wake unategemeana. Kwa mfano: huwezi kufinyanga ugali pasipo kiganja cha mkono wako kushirikiana na vidole vilivyo katika kiganja chako.

Acha sasa tuingie katika mada husika. Tunapotembea au kusimama tukiwa wima, inasaidia tusipoteze nishati kwakuwa mtu husimama wima kwa kutumia misuli kidogo tu. Misuli hiyo hasa ndiyo hutusaidia kusimama wima au kutembea kwa madaha bila wasiwasi au tabu yoyote. Namna gani kuhusu kiwango kinachotumika tunaposimama? Ukweli ni kwamba kiwango kinachotumika cha nishati kwenye kusimama kinazidi nishati inayotumika tunapolala kwa 7% tu, hivyo tunaposimama tunatumia nguvu ndogo sana ya nishati.

Skeletal_muscle

Tukijilinganisha na wanyama wa aina nyingine kwa mfano Mbwa, Mtafiti mmoja wa neva Bwana John R. Skoyles anasema kwamba mbwa anaposimama kwa miguu yake minne hutumia 70% zaidi ya nishati kuliko anayotumia anapolala. Jambo hilo linaonyesha jinsi mwili wetu unavyotenda kazi wakati tunaposimama. Hatutumii nishati nyingi kama mnyama huyo.

Kumbuka misuli yetu mwilini hufanya kazi muhimu sana. Lakini huwenda unajiuliza, misuli ni nini?

Hizo ni sehemu za mwili wa wanyama na binadamu zinazowezesha mwendo wa viungo vyake. Msuli unaundwa na tishu ya pekee yenye uwezo wa kunywea na kulegea. Wakati wa kunywea, msuli huwa fupi zaidi. Kwa njia hii, misuli inayounganishwa na mifupa ya mkono au mguu huleta mwendo wa viungo vya mwili.

Bila shaka unajivunia unapopata fursa ya kutembea mwendo mrefu au kusimama wima huku ukiwa na mazungumzo mazuri pamoja na rafiki zako au kufanya shughuli zako. Basi endelea kuutunza mwili wako maridadi sana.

2 thoughts on “MWILI WAKO NI MASHINE YA KIPEKEE SANA. WAJUA KWANINI?

  1. Nimefurahi kujua jambo hili, ckuwa najua mwanzo….asante kwa kutufunza.

    Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s