MAMBO SITA YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA SMARTPHONE NZURI.

Mambo ya kuzingatia tazama kama ifuatavyo hapa chini:-

1. Mobile Hostspot: Hii inamaana kuwa simu inauwezo wa kutumia huduma za wireless yaani Wi-Fi, hivyo unapokuwa sehemu yenye wireless utaweza kutumia internet bila kutumia gharama.

2.Dual Core processor: Inamaana kuwa simu hiyo inatumia Processor mbili na hiyo pia itakuhakikishia spidi ya uhakika wa simu hiyo kwenye ufanyaji kazi tofauti na yenye Processor moja.

3. 4G au 3G : Hii inaonyesha uwezo wa ufanyaji kazi wa simu kwenye mtandao wa internet. Ila kumbuka kunatofauti kubwa kati ya 4G na 3G hasa kwenye spidi ya internet. 4G ina spidi mara kumi zaidi ya 3G hivyo hapa uchaguzi ni wako.

4. Memory Card (MicroSD): Hii ni memori unayoweza kupachika katika simu yako na kuongeza uwezo wa simu kutunza vitu vyako. Sasa zingatia sana uwezo wa simu kama inauwezo wa kupachika hiyo memori au la. Ni bora kununua yenye uwezo wa kuendesha memori kubwa mfano 32GB au zaidi kwakuwa simu nyingi zinakuja zikiwa na 4GB.

5. Megapixel: Hapa nazungumzia uwezo wa kamera ya simu, na kuna simu nyingi siku hizi zinajaribu kuiga aina fulani za simu kwa kudanganya uwezo wa kupiga picha kwa simu zao. Fanya hivi, kabla ya kununua fanya jaribio hili: washa simu kisha nenda sehemu ya kamera na jaribu kutazama muonekano wa picha kwenye kioo hapo utagundua kama ni nzuri au la. Pili, piga picha angalau moja au mbili kupata uhalisi. Kumbuka, Megapixel ikiwa kubwa ndivyo ubora wa picha unaongezeka.

6. Screen: Hiki ni kioo cha simu. Ni muhimu sana kutazama kwani kuna aina nyingi za vioo hivyo, kuna unavyoweza kugusa kwa kutumia nguvu nyingi na unavyoweza kugusa bila kutumia nguvu yaani vina hisi ya hali ya juu. Hiki cha pili ndicho kilicho bora zaidi. ‪#‎IDEA‬+

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s