BAADA YA WEAKLEAKS SASA NI AFRILEAKS TOKA BARANI AFRICA

Mtandao mpya mfano ule wa Wiki Leaks , unaolenga kutangaza visa vya ufisadi umezinduliwa barani Afrika. Mtandao huo kwa jina ‘Afri Leaks’ unanuiwa kutumiwa kulinganisha na kutangaza wazi visa vya ufisadi katika bara nzima.

Kile Afrileaks inaahidi ni mfumo wa hali yajuu wa kama posta mtandaoni ambapo mtu anaweza kuutumia kufichua habari za siri lakini muhimu kwa jamii bila wao wenyewe kujulikana.

Mwenye habari nyeti ataweza kuzipeleka kwa vyombo vya habari kote barani Afrika ambavyo wamejiridhisha navyo kwamba viko huru na wana uhariri wa hali ya juu unaotambulika kimataifa.

Mojawapo ya Maswala yanayowakera wengi ambayo huenda yakapata kuchipuliwa kwa wingi iwapo mfumo huo wa Afrileaks utafana , ni kashfa za ufisadi.

Licha ya kuwa na viwango vya kuridhisha vya ukuaji wa uchumi,Mataifa mengi ya Afrika hata yale yaliyo na utulivu wa kisiasa hupoteza mabillioni ya fedha kila mwaka kutokana na ufisadi uiokithiri, huku taasisi hafifu zikibuniwa bila kuwa na nia ya dhati ya kukabiliana na rushwa. .

Lakini Je Afrileaks wataweza kupata umaarufu kama ule wa wikileaks?

Shirika hilo la Afrileaks linasisitiza kuwa halitachapisha habari zozote za kibanfsi za mfichua siri.

Na kwamba lengo lao ni kuwaunganisha wenye taarifa muhimu na waandishi habari wanaoandika makala zilizopelelezwa na kuchunguzwa kwa kina. Pia wameahidi kutoa mafunzo zaidi kwa waandishi habari waliobobea ili kufahamu vyema vipi kuzishughulikia taarifa kama hizo.

Habari zaidi tembelea http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2015/01/150113_afrileaks_?SThisFB

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s