WAWEZA KUONGANISHA SIMU YAKO NA KUWA SECURITY CAMERA. 

Karibu tena kwenye page hii ili tujuzane zaidi. Kupitia simu yako unaweza kufanya mambo mengi zaidi na hapa nazungumzia simu aina ya smartphone. 
Simu yako waweza kuifanya iwe security camera na hivyo kukuwesha kurekodi matikio kadhaa iwe ni ofisini kwako au nyumba kwako, mbinu hii haigharimu pesa nyingi kama mifumo mengine na waweza kuifanya mwenyewe. 

Sasa niwaeleze kwa ufupi nini kitahitajika/unachopaswa kufanya hapa ili ufanikiwe. Kwanza uwe na kompyuta aina yoyote, pili modem na tatu simu. Hakikisha simu yako na modem ina kifurushi cha Internet. Sasa kwenye simu yako ingia kwenye Google playstore na download app inayoitwa IP Camera na u-install kwenye simu yako. Baada ya kufanya hivyo pachika modem kwenye kompyuta na fungua browser yoyote kisha utaandika address ukianza na http:// kisha kuna namba za IP utakazozipata toka kwenye app uliodownload. 

Utakapoziingiza namba hizo utapata connection kati ya kamera ya simu na kompyuta na hapo utaweza kukontro kamera ya simu kupitia kompyuta yako na kisha tegesha simu yako sehemu unayotaka kurekodi matukio. 

Ikiwa una swali au maoni unakaribishwa sana. Tupo kusaidiana.

SAMSUNG YAKABILI TATIZO LINGINE KWA TOLEO LA NOTE 2 BAADA YA NOTE 7

​Wafanyikazi wa kampuni moja ya ndege nchini India walilazimika kutumia kifaa cha kuzima moto ili kuizima simu aina ya Samsung iliokuwa ikifuka moshi.

Simu hiyo ya Note 2 ilikuwa ikitoka miale ya moto kulingana na taarifa kutoka kwa kampuni ya ndege ya Airline Indigo.

Hatua hiyo ya haraka iliochukuliwa na wafanyikazi hao ilisaidia ndege hiyo kutua salama katika uwanja wa ndege wa Chennai,ikiwa ndio lengo la safari hiyo.

Kisa hicho kimetokea wakati ambapo Samsung inazirudisha simu aina ya Note 7 kutokana na matatizo ya betri. 

IndiGo imesema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa wakati wa kisa hicho katika ndege ya 6E-054 iliokuwa ikitoka Singapore kuelekea Chennai. 

Source BBC 

Laptop Yenye Kioo Kilichopinda 

​Kampuni ya Acer imezindua laptopu ya kwanza ilio na kioo kilichojipinda.Acer inasema kuwa uvumbuzi huo utaiwezesha kucheza michezo ya video.

Televisheni kadhaa pia zimetumia uvumbuzi huo,lakini umezua mgawanyiko kwa kuwa una umuhimu na ubaya wake.

Kampuni hiyo ya Taiwan pia ilitangaza kwamba imefanikiwa kupata tekenolojia ya pet katika mkutano na wanahabari mjini Berlin.

Kampuni kadhaa za kielektroniki ikiwemo Samsung,Lenovo,DJI,Sony na Huawei zinatarajiwa kuzindua sura mpya ya laptopu zake katika maonyesho ya kiteknolojia ya Ifa katika mji mkuu wa Ujerumani wiki hii. 

Laptopu hiyo ina kioo kikubwa ikilinganishwa na laptopu ya kawaida ya Acer,lakini ni umbo lake ambalo liliifanya kampuni hiyo kudai kuwa ya kwanza kuzinduliwa duniani.

Source BBC 

USICHOKE TENA WAKATI WA KUMBEMBELEZA MTOTO!  

Hapa nimebuni njia rahisi ya kukupunguzia uchovu wa kumbembeleza mtoto. Ni njia rahisi sana unaweza kuifanya ukiwa nyumbani kwako.  

Unahitaji kuwa na vitu vifuatavyo:-

1. Kengele ya kawaida ya kuchezea watoto. 

2. Vibrator hii unaweza kuipata kwenye simu mbovu. 

3. Betri ya simu. 

4. Super glue. 

5. Uzi wa kushonea. 

Utakapoonganisha vitu hivyo utakuwa umepata kengele ambayo utaweza kuiwasha na kwanza kujichezesha yenyewe ili kumbeleza mtoto.  Hakikisha unafunga kengele kwenye Uzi ule wa kushonea na kuining’iniza jirani na mtoto ili itoe sauti vizuri. 

Ikiwa una maoni au ushahuri unakaribishwa. Asante kusoma. 

Sasa tazama picha chache hapa chini

SIMU YAKO IMEFUNGIWA? USIITUPE UNAWEZA KUITUMIA KWA KAZI HII.

Hapa kuna njia mpya ya matumizi ya simu iliyofungiwa.  Unaweza kutumia simu yako hiyo kuwa taa ya kuchaji, mmmmh uwenda imestuka kidogo. Uwe na hakika inawezekana bila tatizo lolote. 

Unahitaji kuwa na taa za LED hizi zinapatika kwa gharama nafuu Kuanzia shilingi 5,000/= na kundelea uwenda katika eneo lako ikawa nafuu zaidi, unaweza kuzipata kwa machinga. Utakapofanikiwa kuonganisha kila kitu basi taa yako itaweza kudumu kwa saa 3 hadi 4 ikitegemea uwezo wa betri ya simu yako.

Sasa tazama picha chini kwa msaada.. Ila ukiwa na swali au maoni unakaribishwa, tupo kwa ajili ya kusaidiana mawazo yako muhimu kwa wote. Asanteni.

Je, Ungependa Kutumia Flash Disk kwenye Simu Yako?

​Uwenda ikakushangaza kidogo, hata hivyo jambo hilo linawezekana kabisa bila shaka yoyote. Tazama picha chini.

Unachotakiwa kufanya ni kununua usb cable yenye kichwa kama ya za port ya computer wakati huo ule upande mwingine ikiwa inauwezo wa kuingiliana na simu yako.

Kwa simu nyingi hasa zenye uwezo mkubwa wa betri kama 4000 mAh, 5000 mAh na kuendelea huja na usb caple mbili moja kati ya hizo hutumika kugawa charge kwa simu nyingine kwakuwa uwezo wa betri hizo huwa ni mkubwa sawa na kifaa kinachoitwa power bank.  

Tazama picha kwa msaada zaidi. Na uta enjoy vitu vilivyo katika flash disk yako kwa kutumia simu yako ya mkononi, pia kuamisha files au picha zako kutoka kwenye simu na kuweka kwenye flash disk. Kama kuna swali au maoni karibu sana.

JE, UNGEPENDA KUWEKA BOLD & ITALIKI KWENYE UJUMBE WA WHATSAPP?

Watu wengi husumbuka sana wanapoandika ujumbe kwenye mtandao wa WhatsApp kutokana na hali kwamba herufi huwa na uzito sawa wa rangi katika hali ya kawaida. Aidha, mtindo wake huwa mmoja.

Je, wajua unaweza kukoleza rangi ya herufi na kuzifanya nzito (bold), ukaziweka kwa mlazo (italiki) na pia ukaweka mstari unaozikata herufi kati, kwa Kiingereza strikethrough?

Unachohitaji kufanya kwanza kabisa ni kuwa na toleo la karibuni zaidi la app ya WhatsApp kwenye simu yako.

Kuweka bold
Ili kukoza rangi kwenye herufi (kufanya bold), unahitajika kutanguliza neno lako na alama ya nyota na kisha kuhitimisha na alama ya hiyo hiyo nyota.

Kwa mfano, ukiandika *bold* itatokea ikiwa bold

Kuweka italiki
Ili kufanya herufi zako kuwa za mlazo au kuwa za italiki, unahitajika kutanguliza na mstari sakafu (underscore) na kuhitimisha na alama iyo hiyo.

Ukiandika _italics_ itatokea ikiwa italics

Kuweka underscore
Ukitaka kuweka alama ya kukata kati kwenye herufi zako, unahitajika kuanza na alama ya mawimbi au kwa Kiingereza tilde (~) na kuhitimisha na alama iyo hiyo.

Ukiandika ~strikethrough~ itatokea ikiwa na mstari uliokata herufi kati.

Kuunganisha mitindo
Unaweza ukataka kuunganisha mitindo, mfano utake kuwa na bold na italiki.

Utahitajika kutumia alama za unachohitaji katika kuanza neno lako na kuhitimisha.

Mfano, ukiandika _*bolditalics*_ inafaa kutokea ikiwa bolditalics.

#SourceBBC